Na Mosses Benedict
Mawasiliano +255 762 371 383
MAELEKEZO; Somo hili tutatembea nalo taratibu kwa kadri ya neema ya Mungu na mfululizo nilionao ndani ya moyo wangu. Yesu ni halisi na anasema Nenoi halisi ivo na hili somo hili halisi kabisa. Fuatilia somohili kila wiki kwa mfululizo tutakao kuwa nao kwa kadri ya majibu ya Mungu kwa watu wake hasa waliolemewa katikam kuishi. Omba kila usomapo hatua na msihi Mungu azidi kukufundusha katika Roho mtakatifu.
MATHAYO 11:28-30, Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na
mzigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa
mimi ni mpole na
mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa
maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi
Lengo kuu la somo hili ni;
kuongeza kiwango cha uhuru ndani ya moyo wako kwa kuona Yesu akikutua mizigo
unayopitia katika hali ya maisha yako, pamoja na ;
1.
Kujua kuwa kuna matatizo, shida,
fedhea, aibu, taabu na au misiba iliyo ndani ya uwezo wako na iliyo nje na
uwezo wako, na licha ya kuwa na watu wa kukuombea na kukushauri lakini ni mmoja
tu wa kukusaidia katika yote ni mmoja tu yaani Yesu.
2.
kujua kuwa unaweza kufikia katika
maisha yako na ukamwambia Mungu niue kama Eliya na hakuui, nitoe mahali hapa au
nitoe katika kanisa hili, eneo, ofisi na hakutoi ila anaondoa tatizo
lililokufikisha katika hali uliyomo na anakuacha hapohapo katika eneo lako,
familia na au ukoo kama ulivyokuwa. Maana yake anaondoa kinachokutesa,
kinachokuumiza, kinachokupa shida, aibu, fedhea lakini wewe hakuondoi.
3.
Kujua kuwa kuna vyanzo mbalimbali vya
kukupelekea kuingia katika hali ya majuto, vilio, kuugua nafsini mwako,
magonjwa, kutozaa, kutoolewa au kutooa, kutofanikiwa lakini suluhisho la maisha
yako ni ufunguo mmoja tu.
4.
Somo hili linalenga kukufundisha kuwa
kuna kutazama shida uliyonayo kwa kujilinganisha na kanisa lako, kikundi au
chama chako, mazingira, familia au ukoo, kaya na jamii, kundi rika na bado
vipimo vya namna hii havizai utatuzi wa shida yako. Kwaiyo tazama kila tatizo
kwa jicho la Yesu ndo utapata utatuzi kwa ajili ya maisha yako.
5.
Pia ndani ya somo hili andaa akili,
ufahamu na fikra zako ili kujifunza namna ya kutua mzigo ili naye akusaidie
kukutua mzigo, kwaiyo ujiandae kuwajibika wewe binafsi kumwendea Yesu maana
yake onesha hali ya kuhitaji msaada kuwa wewe peke yako hauwezi.
Kwaiyo somo hili linakulenga wewe ndugu
katika Kristo ambaye umefikia mahali au katika hali fulani kimaisha labda
katika; ofisi unayofanyia kazi, mahangaiko ya uchumi, uhusiano na ndugu, mwenza
au rafiki, huduma na utumishi, ugonjwa wa mda mrefu, pito fulani linalokuhumiza
kila siku, linakusumbua hadi umefika hatua kila ukilala unaona tatizo
hilohilo kiasi cha kukosa furaha ya kuishi, umechoka, umehaibika, unajionea
aibu, fedhea, hufai, umejikana, umefika hatua ukajitamkia vibaya lakini sikia
Neno la Bwana, katika hali hiyo ya
kulemewa Yesu anakwambia ivi njoo nikutue mzigo. Umesikia Bwana Yesu
anavyokwambia, nakuuliza umesikia? Soma hili andiko ukaone. Mathayo 11:28-30,
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye
kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu;
kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini
mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu!
Haleluya haleluya.
Naomba turudi katika kichwa cha somo
letu cha namna ya kumtwika Yesu fedhea uliyonayo, na tuanze
kuangalia kadri ya neema ya Mungu aliyehai katika Kristo Yesu;
Fedheha;
ni hali ya aibu inayompata mtu kwasababu ya aidha tukio lililompata, hali
anayopitia au matendo aliyoyafanya au aliyofanyiwa lakini kwa ujumla yeye
binafsi anajishuhudia au anajionea aibu kwake binafsi, familia na kwa mwana
jamii anayemzunguka.
Katika hali ya namna hii unaweza
ukajiona au ukajihisi katika mazingira na hali ya namna tofautitofauti saana,
ukawaza saana, ukapoteza mwelekeo wa maisha au tumaini. Ukajiona au ukajipangia
vibaya, ukaona giza tupu mbele yako, ukaona hufai hata katika lolote kwa jinsi
ya kibinadamu tena ukafikia hatua ya kujificha kwa marafiki zako, ndugu na
jamii inayokuzunguka kwasababu ukitazama msiba ulionao, ugonjwa wako, taabu na
shida ulizonazo, au hali uliyonayo vinakuzalia aibu, huzuni, majuto,
masikitiko, fedhea, kujilaumu kwamba kwanini mimi ndani ya moyo na nafsini
mwako.
Na Yesu anapokujia wewe uliyelemewa
anataka aondoe yote hayo ndani ya nafsi yako na akupe raha nafsini mwako,
amani, furaha, utulivu na uone hali mpya katika hali ya maisha yako maana ndiyo
anavyokwambia kuwa atakupa raha nafsini mwako katika Mathayo 11:29, Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu
Bwana yesu asifiwe! Bwana wetu Yesu
Kristo asifiwe.
Kwaiyo kulingana na maandiko
tunayotembea nayo, weka akili mwako hili jambo muhimum kuwa kuna watu wana
mizigo, aibu, fedhea lakini bado haijawatesa kwa kiwango cha kuwalemea na ivo
Yesu hajawatua mizigo yao, aibu na fedhea zao kwasbabu vitu walivyonavyo aidha
ni vya kawaida, au wamepungukiwa tu na nguvu za kuwasaidia kubeba walivyonavyo
ila mizigo hiyo iko ndani ya uwezo wao kabisa, au wamebeba vibaya, au wanataka
kutua tu bila sababu na ivo Yesu anasema subiri kidogo kwanza mpaka ulemewe ndo
uje kwangu nikutue mzigo wako.
Unaweza ukasema niue kama Eliya, lakini
ujue Eliya hakusema niue kwasababu rahisi rahisi tu ni baada ya kuona hali na
mazingira yote yamekuwa magumu kiasi ambacho hatamani tena kuishi na kama vile
yamefika mwisho, unaweza ukamwambia nitoe katika njia hii au nitoe katika hali
hii maana nimechoka na nimelemewa kama Yesu wakati wa kuelekea msalabani lakini
hakuoi bali aidha anakutia nguvu za kukusaidia kutembea au anaondoa unachokiona
ni tatizo kwako lakini wewe anakakuacha hapohapo. Haleluya! haleluya mtu wa
Mungu aliyehai
Karibu katika somo hili, tuombeane kwa
Mungu atupaye neema ili tuendelee nalo kwa kadri ya neema yake. Maombi yako juu
ya huduma hii na madhabahu hii ni muhimu mbele za Bwana.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa somo hili
na tutaendelea nalo kila wiki kwa mfululizo nilionao ndani yangu.
Mungu atupe neema, karibu katika
Kristo Yesu.
No comments:
Post a Comment