Kutafakari
uhusiano wa hali ya maisha ya Gideoni na madhabahu aliyokuwa akiitumikia baba
yake ya Baali.
Waamuzi
6:11-32. Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika
Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa
akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. 12 Malaika wa Bwana
akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. 13 Gideoni
akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote
yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu,
wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa,
naye ametutia katika mikono ya Midiani. 14 Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa
uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani.
Je!
Si mimi ninayekutuma? 15 Akamwambia,
Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio
maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba
yangu. 16 Bwana akamwambia,
Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. 17 Naye akamwambia,
Kama nimepata kibali mbele za macho yako, basi unionyeshe ishara, ya kuwa ndiwe
wewe unayesema nami. 18 Tafadhali,
usiondoke hapa hata nikujie, nikatoe zawadi yangu, na kuiweka mbele zako.
Akasema, Nitangoja hata utakaporudi. 19 Basi Gideoni akaingia ndani, akaandaa
mwana-mbuzi, na mikate isiyotiwa chachu, ya efa ya unga; akaitia ile nyama
katika kikapu, akautia mchuzi katika nyungu, akamletea hapo nje chini ya
mwaloni, akampa. 20 Naye
malaika wa Mungu akamwambia, Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uiweke juu
ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi.
Akafanya
hivyo. 21 Ndipo malaika wa
Bwana akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama
na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; malaika
wa Bwana akaondoka mbele ya macho yake. 22 Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa
Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso
kwa uso. 23 Bwana akamwambia
Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa. 24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu
hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya
Waabiezeri. 25 Ikawa
usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa
pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako,
ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; 26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu
juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa
awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. 27 Ndipo Gideoni
akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana
alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake,
na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda
usiku.
28 Hata watu wa mji
walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile
Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka
juu ya ile madhabahu iliyojengwa. 29 Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo
hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi,
ndiye aliyetenda jambo hili. 30 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete
mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile
Ashera iliyokuwa karibu nayo. 31 Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa
wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea
na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu
mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake. 32 Basi akamwita Yerubaali siku hiyo,
akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa
madhabahu yake.
Somo
letu kwa kiasi kikubwa liko ndani haya maandiko, kwaiyo soma kwa kurudia rudia
hii habari kabla ya kuendelea, maana ukipata picha ya hapa itakusaidia saana
tunakoelekea. Haleluya haleluya !!!
Tunapotafakari
kwa kuangalia mambo kadhaa juu ya hali ya ndugu huyu kulingana na maandiko,
nawe pia jipime au jitazame kama uko ndani ya hali au mazingira ya namna hii au
laah!! Weka picha ya maisha ya Gidioni katika mazingira ya uhalisia kwamba haya
mambo yapo kwa kutazama wewe binafsi, familia, majirani, jamaa na jamii
ulipokuwa na ulipo kwa sasa ili upate msukumo ndani yako wa kuona sababu ya
kushughurikia madhabahu au sababu, kiu na hamu ya kutaka kujitoa katika
madhabahu za giza kadri ya utakachopata.
Mambo
ya kutafakari
01. Kazi
aliyokuwa anaifanya Gidioni.
Waamuzi
6:11, Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika
Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa
akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Kulingana
na maandiko yanavyoeleza kijana Gideoni alikuwa pale mwaloni akipepeta ngano
ndani ya shinikizo. Maana yake, kazi yake ilikuwa ni ya kupepeta ngano.
Tunaelewana mpaka hapo ?? Lakini pia eneo, sehemu au mahali alipokuwa anafanyia
kazi hapakuwa eneo lake yaani pale mwaloni, mwaloni uliokuwa Ofra ulikuwa mali
ya baba yake mzee Yoashi. Maandiko hayaweki wazi kama alikuwa anapepeta ngano yake
binafsi au ya baba yake yaani familia.
Mungu
alipomuumba Gideoni kuna kiwango cha hali ya maisha alichokikusudia akiishi cha
kumtukuza Mungu ambacho hicho kiwango kinaambatana na aina ya kazi ya kufanya
inayoendana na hali ya maisha yake katika mifumo yote ya maisha, mfano- uchumi
wa mtu binafsi.
Kazi
aliyokuwa akiifanya Gideoni ilikuwa kama kazi isiyokuwa na thamani, heshima,
isiyokuwa na kipato, kazi ya kudharauliwa, kazi za watu masikini au kazi za
vijana wa hali ya chini kiuchumi. Sasa fikiri kazi za namna hii na maisha yako
binafsi, familia, kundi rika au jamii na piga picha kazi uliyonayo. Pia jiulize
wewe kazi yako ni ipi?
Mungu
alipotaka kumtoa katika hali ya maisha ya namna hii alimpa jukumu la kufanya
ili hali ya maisha yake yabadirike. Gideoni aliambiwa kubomoa madhabahu
aliyokuwa nayo baba yake? Kwanini abomoe madhabahu ya baali ya baba yake? Kwa
sababu madhabahu ya baba yake kama mkuu wa familia ilikuwa inatengeneza hali ya
maisha ya wana familia wote akiwemo Gideoni, ivo kama Gideoni akitaka kutoka
katika hali ya namna hiyo ilimlazimu kuvunja, kubomoa na kuharibu madhabahu
inayohusika na kiwango cha hali ya maisha yake.
02. Umasikini
wa familia nzima.
Waamuzi
6:15, Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi
gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi
ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
Mazungumzo
ya Mungu na Gideoni yalivyokuwa yanaendelea, Gideoni alikuwa anajaribu kuelezea
hali halisi ya maisha yake binafsi pamoja na familia yake. Anasema hivi; jamaa
zangu ndio masikini sana katika kabila ya Manase. Maana yake kabila la Manase
lilikuwa na familia au kaya tofauti tofauti zenye hali tofauti kimaisha hasa
kiuchumi, na kaya ya ndugu za Gideoni ilikuwa masikini saana katika eneo hilo.
Alipojibu
kuwa ndugu zangu ndio masikini saana, alimaanisha kuwa ndani ya familia yao
wote ni masikini hakuna cha dada wala kaka, mkubwa wala mdogo woote ni
masikini. Kwakuwa ni masikini saana basi hata hakuna atakaye msaidia kifedha
katika masuala ya huduma na utumishi.
Kwa
jinsi ya sasa ni aina ya umasikini ambao; unashinda shule lakini katika ndugu
wote hakuna wa kukusaidia, mmojawapo akiumwa ndugu wote wanasukumana tu na
mgonjwa anaweza akapoteza maisha kisa ndugu wote hawana kitu, ukipatwa na kesi
ghafla unakosa hata wa kukuthamini na unafugwa kwa sababu ya kukosa pesa tu
ambayo ni ya kawaida kabisa, familia nyingine ukizitazama ni kama vile hakuna
mkubwa na mdogo, ndugu wote wameishia darasa la saba, hawakusoma shule au
hawakuimaliza na hawana pa kushikilia n.k
Tazama,
jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, maana yake familia yake
ni familia ambayo haina sauti pale kijijini, mjini, kanisani n.k. Au ni familia
ambayo haina nafasi, haisikilizwi, inadharauliwa. Sasa kwa kujua ivo akilini
mwake alijua kabisa kuwa hata kama Mungu akimtuma bado yeye hatasikilizwa na
jamii kwasababu wanaweza wakamdharau kwa sababu ya umasikini wake. Bado hii sio
sababu hata kwako leo!!!
Sasa
sikia, kilichotengeneza familia nzima kuwa masikini tena sana ni kitu gani? Maisha
ya hapa duniani yanaamuriwa kwa kiasi kikubwa na madhabahu tunazozitumikia ivo
madhabahu ya mzee Yoashi ilihusika na hali ya maisha yake binafsi pamoja na
familia yake yaani hali ya maisha ya watoto wake. Na Mungu alipotaka kumtoa
katika hali ya umasikini uliokithiri namna hiyo alimwambia madhabahu. Unasikia
ninachosema?? Nasema madhabahu zinatengeneza hali ya maisha kwa watu walio
chini ya hiyo madhabahu husika.
03. Kujidharau
kiumri kwa ngazi ya familia kulingana na mira na desturi za jamii.
Waaamuzi
6: 15, Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama,
jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye
mdogo katika nyumba ya baba yangu.
Gideoni
anamjibu Mungu kuwa, katika ndugu zangu wote mimi ndiye mdogo katika nyumba ya
baba yangu. Akijaribu kumaanisha kuwa kulingana na mira na desturi za familia
yetu, ukoo au kabila kuna baadhi ya kanuni, taratibu, sheria, mienendo na miiko
ambayo tunaifuata na mojawapo ni mtu aliye mdogo kutofanya jambo fulani ambalo
wakubwa zake bado hawalifanya na kwasababu hiyo eeh Bwana nakuomba hii kazi
ukawape wakubwa wangu.
Mwanzo
29:25-26, Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani,
Nini hii uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani
akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa;
Unaona
kitu alichofanyiwa Labani hapa kulingana na tamaduni za jamii ile? Yeye
alifanya kazi miaka saba kwa mzee Labani ili baada ya mda huo apewe binti
aliyekuwa amempenda kwa uzuri wake lakini baada ya miaka yooote saba hakupewa
huyo binti mdogo mzuri bali alipewa dada yake aliyeitwa Lea. Na Yakobo
alipouliza kwanini amefanyiwa mchezo wa namna hiyo, aliambwa hivi; havitendeki
hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa. Kwa maana nyingine kulingana na tamaduni
zao inabidi kuolewa au kuoa aliye mkubwa kwanza kabla ya mdogo. Vipi wewe
kwenyefamilia au jamii kuna mira za namna hii? Jiulize ni wewe hapo umemaliza
miaka saba alafu unaambiwa kijana umechemka aisee! Kisa ni tamaduni.
Nadharia
ya namna hii ilimfanya hata Gideoni alipotokewa na malaika kutaka kukataa wito
wake ambao ndo utakaobadirisha maisha ya baadae kwa sababu ya umri. Kumbuka hii
ilikuwa ni fursa ya kubadirisha maisha yake kwa msaada wa Mungu aliyehai.
Mazingira
ya namna hii yalitengenezwa na wakuu wa eneo, wazee, washauri au wazee wa
busara wa eneo hilo ambapo baadhi yao au miongoni mwao walikuwa wanatumikia
madhabahu za giza kama mzee Yoashi, ivo hofu au utii wa tamaduni za namna hii
haukuwa kwa jinsi ya mfumo wa Mungu aliyehai bali chimbuko lake lilikuwa ni
madahabahu za giza. Ndo maana Mungu alimwagiza Gideoni kuondoa kwanza
kinachoachilia roho za kujidharau, kujiona huwezi kulingana na mira na desturi
zenye kulenga kukubana ndani yake. Bwna Yesu asifiwe!! Haleluya haleluya.
1Samweli
16:6-13, Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa
BWANA yupo hapa mbele zake. Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso
wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama
binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana
huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli.
Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye
akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya
Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha Samweli
akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao,
na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu,
wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi akatuma mtu, naye
akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake
lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake;
na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli
akaondoka, akaenda zake Rama.
Hapa
unaona jambo lililotaka kutokea kwa Daudi, Mungu alimchukulia Daudi tofauti na
wengine walivyomchukulia kwa sababu za kwao wenyewe za kibinadamu. Kuanzia kwa
baba yake pamoja na mtumishi mwanzoni alipofika ndani ya nyumba ya mzee Yese.
Hawakutambua mapema kitu kilichokuwa juu ya Daudi kwa ajili ya Bwana, nah ii
ilisababisha huyo motto, kuishi katika mazingira aliyokuwemo mpaka mkono wa
Bwana ulipodhihirishwa juu yake, na mkono wa Mungu ulikuwa tofauti na mazingira
aliyokuwa akiishi pamoja na nje ya akili za baba yake pamoja na mtu wa Mungu.
Hata wewe Mungu anakutazama tofauti na mira, desturi au mazingira uliyomo.
Kwaiyo
maisha ya kifamilia au ndoa ya binti Lea kidogo yakwamishwe na mira na tamaduni
za ukoo wao, maisha ya Daudi ya utumishi na ufalme yaani kulitumikia kusudi la
Mungu kidogo pia yakwamishwe na mtumishi, ndugu akiwemo baba yake pamoja na
mazingira, maisha ya Gideoni kidogo yalikwamishwa na baba yake pamoja na
mazingira. Mira na desturi au tamaduni za kifamilia, ukoo, kabila au eneo na
jamii ilitaka kukwamisha maisha ya hawa ndugu ya hapa duniani. Lakini Mungu
wetu azuiliwi na mambo ya tamnaduni, kwaiyo nawe haijalishi unazuiwa na jambo
gani la kiutamaduni lenye muunganiko wa kimadhabahu, bado Kristo yupo kwa ajili
yako.
04. Thamani
ya Gideoni.
Waamuzi
6:11-12, Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika
Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa
akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. Malaika
wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa
Hapa
tunaona thamani ya Gideoni katika mazingira mawili tofauti, maisha yake ya
mwilini hapa duniani na maisha yake ya kiroho yaani mbinguni.
v Thamani
ya Gideoni hapa duniani. Thamani yake hapa duniani ulikuwa ya chini saana
kwasababu ya umasikini wake pamoja na familia yake kwa ujumla. Hii
ilimsababisha yeye kujiusisha na shughuri za kudharauliwa, kazi zenye pato dogo
au zenye faida ndogo. Maisha yake ya hapa duniani yalikuwa ya taabu saana,
shida, mihangaiko nay a nguvu saaana kiasi yeye binafsi kujiona si kitu katika
maisha haya kwa familia, ndugu, kabila na jamii pia. Maana ni kama vile alikuwa
na thamani ndogo mno kiasi kwamba ni kama vile hana thamani yoyote hapa
duniani. Unajua mbinguni walimwonaje?
v Thamani
ya Gideoni kule mbinguni. Mbinguni walipomtazama Gideoni walimwonaje? Malaika
wa Mungu, wenye uhai wanne, wazee 24, watakatifu na Mungu mwenyewe alimwona
Gideoni mtu mmoja mkubwa mno kule mbinguni, mwenye mafanikio, mshindi, mwenye
maisha ya hali ya juu saana, mtumishi mmoja mkubwa mno, mtu aliyefanikiwa.
Thamani aliyokuwa nayo GIdeobi kule mbinguni ilisababisha serikali ya mbinguni
kutuma mwakilishi wao yaani malaika wa kuja kumwambia kuwa; Bwana yu
pamoja nawe, Ee shujaa. Unasikia ewe shujaa? Unajiuliza nani shujaa hapa
kwa kushanga !!!! ni wewe shujaa wa leo uliyembeba Kristo ndani yako. Bwna Yesu
asifiwe! Bwana Yesu asifiwe!
Kwaiyo
Gideoni alikuwa na thamani mbili tofauti. Maisha aliyopangiwa kuishi tangu
kuumbwa kwake toka mbinguni ni tofauti saana na maisha aliyokuwa akiishi hapa
duniani. Na hakujua kuwa yeye mbinguni anaitwa shujaa mpaka neema ya Mungu
ilpokuwa juu yake, alijishangaa kuona mbinguni wanamwita yeye kuwa ni shujaa.
Inawezekana nawe unaishi maisha kama ya Gideoni tena na kuzidi lakini maadamu
umeokoka na kumpokea Kristo Yesu sikia neno hili, wewe ni mtu mkubwa saana na
una thamani kubwa mno na ushujaa ulio juu yako ni zaidi ya ule wa Gideoni maana
we uko ndani ya agano jipya. unasema sasa mbona niko naishi maisha ya namna hi
indo maana unajifunza somo hili ili ukajinasue katika hali yako na ukawe huru
kwa jina la Yesu. Haleluya Haleluya
Mariko
11:1-10, Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili
mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni
mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara
mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. Na
mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara
atamrudisha tena hapa. Wakaenda zao, wakamwona mwana-punda amefungwa penye
mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. Baadhi ya watu waliosimama huko
wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda? Wakawaambia kama Yesu
alivyowaagiza, nao wakawaruhusu. Wakamletea Yesu yule mwana-punda,
wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake. Watu wengi wakatandaza
mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani. Nao watu
waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye
kwa jina la Bwana; umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu
mbinguni.
Ukisoma
haya maandiko ndani yake kuna vitu vya ajabu mno, unaona thamani ya mwana-punda
katika mazingira mawili tofauti. Licha kuwa ndani ya haya maandiko kuna unabii
wa kipekee aliokuwa akiusema Yesu, lakini tuangalaie hasa juu ya thamani ya
mwana- punda. Tunaona punda akiwa na thamani mbili tofauti; moja ni katika hali
ya kufungwa akiwa amefungwa kule ndani kijijini na thamani yake ya pili ni ile
aliyoipata alipokuwa na Yesu au alipopandwa na Yesu. Hizi ni thamani mbili
tofauti kabisa, uanelewa jambo nasema hapa? Kuwa thamani yako kabla ya kumpokea
Yesu na baada ya kumpokea umekuwa na thamani ambayo haukuwa nayo kabisa.
Kuna
watu ambao hawakutaka yule mwana- punda afunguliwe ndo maana waliwauliza wale
waliokuwa wanamfungua waliokuwa wametumwa na Bwana Yesu, kuwa “Mnafanya nini
kumfungua mwana-punda?” sijui walikuwa na faida gani katika kufungwa kwa
huyo punda lakini au ni kwa kwanini walitaka yule mwana punda abakie katika
maisha yaleyale ya kufungwa. Kwa maana nyingine hawakutaka punda apate heshima
akiwa pamoja na Yesu, hawakutaka punda atoke katika hali aliyokuwa nayo. Mungu
mwenyewe alipooona vema juu ya aliyemchagua alimtokea kuja kumfungua toka
katika hali ya aliyokuwa nayo na mahali alipokuwa. Sasa unaona picha ya thamani
ya Gideoni mbele za Bwana ilivyokuwa tofauti na mazingira pamoja na jamii hasa
wale waliokuja wakitaka kumwua Gideoni kama wale waliouliza kwanini mnamfungua
huyo mwana-punda?
Tutaendelea
na somo hili kadri ya neema ya Mungu na msukumo, nikukaribishe ndugu katika
Kristo kwa ajili ya kufuatilia somo hili linalohusiana na masuala ya
Madhabahu.
Amen ubarikiwe
ReplyDeleteHongera mtu wa Mungu
ReplyDelete